Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un alitazama jinsi “ndege mpya zisizo na rubani” zikiruka na kuharibu shabaha za majaribio ikiwa ni pamoja na tanki la majaribio, na kuwataka watafiti kuunda AI kwaajili ya magari hayo ambayo hayakuwa na majina bado, vyombo vya habari vya serikali viliripoti Jumatatu.
Picha zilizochapishwa na vyombo vya habari vya Korea Kaskazini siku ya Jumatatu zilionyesha ndege isiyo na rubani nyeupe yenye mikia na mabawa yenye umbo la X ikianguka na kuharibu shabaha inayofanana na tanki kuu la vita la K-2 la Korea Kusini.
Kim, ambaye alipigwa picha kwenye dawati lililozungukwa na washauri, amekuwa akiliboresha jeshi la nchi yake na kukuza uwezo wake wa silaha huku kukiwa na mvutano unaoongezeka na Washington na Seoul.
Kiongozi wa Korea Kaskazini alisimamia jaribio hilo katika ziara ya Taasisi ya Drone ya Chuo cha Sayansi ya Ulinzi cha Korea Kaskazini, KCNA ilisema.
Kim alisema kuwa mwelekeo wa kimataifa wa teknolojia za kijeshi na mapigano ya kisasa unaonyesha umuhimu wa ndege zisizo na rubani katika vita na kwamba jeshi la Pyongyang linapaswa kuwa na vifaa “mapema iwezekanavyo”.