Michezo

Maneno ya baba mzazi kuhusu Mkenya Divock Origi kujiunga na Liverpool.

on

Origi 1Najua headlines za huyu mkali wa soka mwenye asili ya Kenya anaeichezea timu ya taifa ya Ubelgiji kujiunga na Liverpool sio mpya kwa wafatiliaji wa soka lakini sasa baba yake mzazi ameongea na reporter wa TZA Kenya Julius Kepkoech.

Mike Origi Okoth amedokeza kwamba kuna timu nyingine ambayo hajaitaja lakini inamtaka mshambuliaji huyu kama zilivyo Liverpool na Tottenham ambapo pamoja na hayo, amesisitiza kwamba hatma ya Divock ni sharti iamuliwe ifikapo Jumatatu wiki ijayo japo Divock mwenyewe bado hajafanya uamuzi kuhusu uhamisho wake japo Liverpool inabaki kuwa timu yenye nafasi kubwa ya kumsajili Divock.

Tupia Comments