Mix

Bado ni majanga ya ajali za ndege, hii ni ya saa kadhaa zilizopita Marekani.

on

Screen Shot 2014-07-28 at 11.01.18 AMMpaka sasa kuna habari nne kubwa za ndege ambazo zimetokea ndani ya kipindi cha siku 9 zilizopita, kuna ajali ya ndege tatu ambazo ni ile ya Malaysia, Mali na Taiwan ambapo kwenye kisa kilichofata ni cha ndege moja kulazimika kurudi ilikorukia baada ya kijana raia wa Canada kusema ana mpango wa kuilipua nchi yake kwa sababu anaichukia.

Sasa tukio jingine la saa kadhaa zilizopita ni kuhusu ndege ndogo ya abiria ambayo imelazimika kutua kwa dharura ufukweni huko Venice Florida Marekani baada ya kupata tatizo ikiwa angani na rubani kuona hakukuwa na uwezekano wa kufika uwanja wa ndege alikofanya mawasiliano.

Screen Shot 2014-07-28 at 11.23.19 AMKutua huku kwa dharura kumesababisha kifo cha Mwanaume mmoja alikua akitembea ufukweni huku mtoto wake wa kike akijeruhiwa vibaya kwenye hii ajali.

Rubani na abiria wake hawakuumia kwenye hii ajali ila mtoto wa kike ambae anahisiwa kuwa na umri wa miaka 10 ndio ameumia sana na kukimbizwa hospitali.

Tupia Comments