Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro linawashikilia watuhumiwa 56 ambao ni wafanyabiashara ndogondogo (Machinga) kwa tuhuma za kufanya fujo katika barabara ya Masika -Msamvu kwa madai ya kutokubali kuhama katika eneo hilo na kuhamia katika eneo lingine ambalo limetengwa na Serikali.
Taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi Morogoro inasema watuhumiwa hao wamekamatwa baada ya kufanya fujo hizo majira ya asubuhi ya leo disemba 20 mwaka huu.
Awali ayo tv na Millard Ayo .Com ilifika katika eneo hilo na kukuta vibanda vya machinga vimevunjwà Usiku wa kuamkia Leo disemba 20.
Juma Shaibu Mwenyekiti wa Machinga Wilaya ya Morogoro anakili kupata barua ya kuwataka waondoke katika eneo hilo lakini changamoto soko ambalo limejengwa kwa ajili ya machinga (Soko la Machinga Fire) haliendani na matakwa Yao.
Ayo tv na Millard ayo .com inafaendela na jitihada za kuutafuta uongozi wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro ili kutolea ufafanuzi taarifa ya kuondolewa kwa machinga hao.