Kituo cha afya cha Adn care kwa kushirikiana na serikali wamefanya vipimo vya magonjwa mbalimbali bure kwa wananchi 400 wengi wao wakiwa ni kutoka Arusha ambapo idadi ya watu mia moja wana ugonjwa wa presha huku wakifuatiwa na gauti
Kupitia kambi ya uchunguzi matibabu ya ya siku tatu iliyofanyika mkoani Arusha imeelezwa kwamba kuna uhitaji mkubwa wa jamii kupima afya zao Mkuu wa polisi wa wilaya ya Arusha Regina Matagi ameeleza jinsi alivyofanya vipimo zaidi ya vitano bure nakupata elimu
Daktari Agrey mapunda ameeleza jinsi kulivyokuwa na idadi kubwa ya wagonjwa wa presha pamoja na gauti nakueleza unasababishwa na kuwepo kwa kiasi kikubwa kuliko cha kawaida cha tindikali aina ya uriki (Uric Acid)
Katika kambi hii tumehudumia watu takriban mia nne tumegundua watu wengi hawahudhurii kwenye vituo vya afya kwa kuhofia upande wa gharama tunashirikiana na serikali tukawafanyia uchunguzi na kuna wimbi kubwa la magonjwa yasiyo ya kuambukiza”Dkt Mapunda