Kwa mujibu wa Erin Venture Services, Rapa Na Mfanyabiashara Kanye West ameripotiwa kuwa mwanamuziki tajiri zaidi duniani mwaka 2025, akiwa na utajiri unaokadiriwa kufikia dola bilioni 2.77 Sawa Na Kiasi Cha Tsh. Trilioni 7/=
Inaripotiwa, idadi hiyo ya utajiri inatokana muziki pamoja na umiliki pekee wa chapa ya YEEZY na sio siri kuwa Kanye West amepata mafanikio makubwa katika muziki na shughuli zake mbalimbali za kibiashara.
Takwimu hii iliyoboreshwa inakuja miaka michache tu baada ya Forbes kuripoti kwamba hakuwa bilionea tena baada ya Adidas kukata uhusiano naye kutokana na matamshi yake ya chuki.
“Naweza kusema antisemitic sh*t na Adidas hawawezi kuniangusha mimi,”
Inaonekana kama himaya ya Ye inaweza kupanuka zaidi kwani mapema wiki hii, kupitia Instagram yake alitangaza mipango ya kuachia brand ya YEEZY womenswear.
Bila shaka, tangazo hilo pia lilikuja na ujumbe mrefu kuhusu makampuni yote ambayo yamemdhulumu hapo awali.
“Using me to get to get to us. Overcharging our community while ignoring my vision and direction. Stopping the foam runners and Yeezy slides production during COVID only to copy the designs.”