Serikali ya Kenya imedai kiwa ingawa Marekani imekata ufadhili wa dola Mil 15 fedha kwa ajili ya mpango wa amani nchini Haiti haitoathiri maafisa wake walio huko na hawatoondoka
Ujumbe wa amani wa takriban maafisa 900 nchini Haiti, MSS unaongozwa na Kenya ambayo ina maafisa 617 wa polisi.
Lengo la Kenya ni kupeleka maafisa 1000 kwa jumla.
” Madai kwamba Marekani kusitisha ufadhili kwa ujumbe wa amani unaoongozwa na Kenya nchini Haiti, kutaathiri oparesheni hiyo, siyo kweli na hayana msingi wowote,” Msemaji wa Serikali ya Kenya Isaac Mwaura amesema katika taarifa.
Mfuko wa Udhamini wa Umoja wa Mataifa kwa Haiti ulianzishwa Oktoba 2023.
” Ujumbe wa amani wa Haiti, MSS unaoongozwa na Kenya una vikosi vya polisi siyo kutoka Kenya tu bali Guatemala, Jamaica, El Salvador, Bahamas na Belize miongoni mwa mataifa mengine,” Korir Sing’Oei, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje nchini Kenya ameeleza.