Habari za Mastaa

Kwa mara nyingine Kanye West akutana na Donald Trump

on

Rapper Kanye West ameonekana kukosolewa na mashabiki siku kadhaa zilizopita baada ya kuibuka kwenye kipindi cha Saturday Night Live akiwa amevaa kofia iliyoandikwa ‘Make American Great Again (MAGA)’ ambayo ni kauli mbiu ya Donald Trump.

Mashabiki walihoji na kusema kuwa Kanye anam’support  Rais Donald Trump na kauli hiyo inayoonekana kuwa ni ya uonevu kwa Wamarekani, kwa mujibu wa mtandao wa New York Times unaripoti kuwa rapper huyo atakuna na Rais Trump Alhamis ya October 11,2018

Kanye West anaripotiwa kula chakula cha mchana pamoja na Rais Trump ikiwemo na kuzungumza kuhusiana na mchango wa kuwapa ajira vijana wa Chicago na iliwahi kusemekana kuwa Kanye West alizungumzia ishu ya kugombea urais wa Marekani mwaka 2020.

TOP 5: Hizi ndio baadhi ya nyimbo anazozipenda Thomas Ulimwengu

Soma na hizi

Tupia Comments