Volodymyr Zelenskyy anatazamiwa kukutana na Keith Kellogg, Mjumbe Maalum wa Rais wa Marekani Donald Trump kwa Ukraine na Urusi huku kukiwa na msukumo wa Ikulu ya White House kumaliza vita na hii inakuja wakati Trump alimkejeli Zelenskyy mara kwa mara, na kuzua chuki za Ulaya.
Kellogg alisema lengo la safari hiyo ni “kusikiliza” wasiwasi wa Ukraine na kuripoti juu yao kwa Ikulu ya White House.
Trump amemwita Zelenskyy “dikteta” na kumshutumu kwa kufanya kazi “ya kutisha”, baada ya Zelenskyy kusema Trump alikuwa akiishi katika “nafasi ya upotoshaji” iliyoundwa na Urusi.
Wakati huo huo Rais wa Marekani Donald Trump aliwaambia waandishi wa habari siku ya Jumatano kwamba Urusi imeshikilia “kadi” katika mazungumzo ya suluhu nchini Ukraine.
“Nadhani Warusi wanataka kuona vita vikiisha… Lakini nadhani wana kadi kidogo, kwa sababu wamechukua maeneo mengi, kwa hiyo wana kadi,” Trump alisema.
Urusi ilianzisha uvamizi wake kwa Ukraine mnamo Februari 24, 2022. Urusi imeweza kuchukua karibu 20% ya eneo la Ukraine katika maeneo ya mashariki na kusini mwa nchi.
Urusi pia ilitwaa Peninsula ya Crimea ya Ukraine mwaka 2014, na hivyo kulaumiwa na nchi za Magharibi.