Mkutano wa kwanza wa baraza la wafanyakazi la AICC kwa mwaka wa fedha 2024 /2025 umefanyika hii leo jijini Arusha huku ukilenga kujadili masuala mbalimbali yahusuyo utendaji wa kila siku pamoja na kutafuta ufumbuzi wa changamoto mbalimbali zinazowakabili wafanyakazi wa AICC katika shughuli zao.
Akifungua mkutano huo naibu katibu mkuu wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa Africa mashariki Mhe. Balozi Shaib Mussa akatoa rai kwa wafanyakazi kusisitiza ushirikiano katika kazi, kutokufanya kazi kwa chuki wala majungu bali kuzingatia maadili ya kazi na kufanya kazi kwa weledi ilikufikia malengo ya taasisi.
Aidha ameeleza ameongeza kwa kueleza muhimu wa mkutano huo kuwa ni kuibua mambo yasiyofaa kwa taasisi, na changamoto zinazo wakabilj ili kuweza kupata ufumbuzi ili taasisi iweze kutimiza malengo yaliyowekwa na taifa ya kufanya kituo hicho kuvutia wangeni wengi kutoka nje
Pia Balozi Said kupitia kikao hichoakawataka watendaji kuweka kipaumbele kufanya ukarabati endelevuna wa majengo ya mikutano pamoja na kuwaendeleza wafanyakazi kimafunzo na kuzingatia maslahi yao ikiwemo kuongezwa mishahara na upandishwaji wa vyeo. huku akieleza kuwa utoaji wa mafunzo kwa wafanyakazi uvuke mipaka ya nchi ili kwenda kujifunza nchi jirani wanavyo endesha mikutani yao na kufanya kazi
Akizungumza katika mkutano huo Mkurugenzi mtendaji AICC Christine Mwakatobe akaeleza
Mafanikio waliyopata ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa mapato ya kituo, kukuza jina la Tanzania katika secta ya utalii wa mikutano inayokidhi viwango vya kimataifa, ukarabati wa kituo kikubwa cha mikutano cha Nyerere (JNICC), kuboresha maslahi ya wafanyakazi, ununuzi wa vifaa mbalimbali, kuboresha huduma za hospitali ya kituo, pamoja na kuimarisha mifumo ya ndani
Aidha akaeleza changamoto zinazo wakabili katika utendaji ambazo ni pamoja na uchakavu wa majengo na miundo mbinu hususani kumbi za mikutano, uhaba wa kumbi za mikutano inayoweza kuhudumia idadi ya washiriki zaidi ya 1500 pamoja na malimbikizi ya madeni ambayo yanaathiri kituo kujiendesha na kutekeleza kiufanisi mipango iliyojiwekea.
Akaongeza kuwa Kituo kinasimamia na kuratibu maandalizi ya ujenzi wa kituo cha kimataifa cha mikutano cha Dkt Samia Suluhu Hasani (SSH-ICC) huku hatua mbalimbali zimekamilika ikiwemo upembuzi yakinifu, kuwahusisha wadau mbalimbali ili kupata ufadhili wa mradi, kwa kushirikiana na PSSSF menejimenti ya kituo imeandaa Rasimu ya hati ya maelewano, mkataba wa ubia na katiba ya kampuni itakayo simamia uendeshaji wa mradi wa SSH-ICC.