Michezo

#Exclusive: Tumesoma sana ya Magazeti, sasa tuisikilize sauti ya Okwi mwenyewe kuhusu kuondoka Yanga.

on

Screen Shot 2014-08-20 at 8.28.55 PMMganda Emmanuel Okwi harudi tena Yanga na sasa ameweka wazi kwamba anashughulikia mipango yake kwenda kucheza soka la Ulaya >>> Okwi aachana na Yanga mchana kweupe!!!!! >>> Okwi achukizwa na ishu ya DVD ya Maximo <<<< hizo ni baadhi tu ya sentensi kwenye Magazeti mbalimbali ya Tanzania kwa wiki kadhaa ila ukweli kutoka kwa Okwi mwenyewe ni huu hapa chini.

Akiwa Kampala ameongea kwenye Exclusive interview na Bill the African ambae ni ripota wa millardayo.com na AyoTV Kampala Uganda na kusema haya >>> ‘Mimi na Yanga tulikua na makubaliano ya mkataba na hakuna ukweli kwamba Mshahara niliokua nalipwa Yanga ni mdogo, mshahara usingekua unatosha nisingekubali kusaini mkataba

Ni kweli kuna mambo mengi hayapo sawa kati yangu na club yangu ya Yanga ila ni mambo ya ndani ambayo nisingependa kuyazungumzia, ni mambo madogo ambayo nadhani yanaweza kuisha

Hakuna ukweli kwamba mimi nakwenda Ulaya, sijui hata imetoka wapi na nani kaanzisha hii ya Ulaya, mimi bado ni mchezaji halali wa Yanga na huwa naongea nao karibu kila siku, hata jana nimetoka kuongea na katibu mkuu na mambo yote yanaelekea vizuri hamna shida yoyote mpaka sasa hivi

Kama unahitaji zaidi kupata ushahidi wa sauti yake Okwi akiongelea hi iishu bonyeza play hapa chini.

Unaonaje kuhusu uwepo wa Okwi Yanga na alichokizungumza leo? niachie comment yako hapa chini mtu wangu na Okwi mwenyewe atapita baadae usiku kuisoma pia.

Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu na niko tayari kukutumia wakati wowote iwe usiku au mchana iwapo utakua umejiunga na mimi kwa kubonyeza hapa >>> twitter Insta FB

Tupia Comments