Top Stories

Aliefukua kaburi la Baba yake awakimbia Polisi Mahakamani, akarudi kaburini (+video)

on

Mtuhumiwa wa shtaka la kufukua kaburi bila ya kuwa na kibali, Joseph Salun (28) mkazi wa Kijiji cha Makiwaru Ngalitati katika Wilaya ya Siha Mkoani Kilimanjaro alifanikiwa kuwakimbia askari akiwa katika eneo la Mahakama kabla ya kukamatwa tena.

Salun kabla ya kuwatoroka askari alifikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Siha kwa ajili ya kusomewa shtaka dhidi yake la kufukua kaburi la baba yake mzazi aliyezikwa miaka mitatu iliyopita kwa kile alichodai kutaka kuchukua blanketi kwa ajili ya kujisitiri na baridi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Hamisi Issah amesema mtuhumiwa huyo baada ya kufanikiwa kutoroka alirudi kwenye kaburi alilolifukua mwanzo kwa kile kinachodaiwa kutaka kuendelea kutafuta blanketi alilolieleza awali.

DC HAI “RAIS MAGUFULI ALITUITA IKULU, AMEAGIZA MSIMDHURUMU MTU KWA JINA LAKE”

Soma na hizi

Tupia Comments