Habari za Mastaa

“Miaka 14 si mchezo, mambo kama haya niliyamiss”-Papii Kocha

on

Leo January 22, 2018 Nikusogezee stori kuhusiana na Muimbaji wa muziki wa Dance hapa Bongo, Nguza Viking maarufu kama Babu Seya na mwanae, Papii Kocha good news ni kwamba wameanza maandalizi ya ujio wao mpya, ikiwa ni takriban miaka 14 tangu waachie kibao kipya.

Babu Seya na Papii Kocha walipewa msamaha na President JPM  kwenye maadhimisho ya miaka 56 ya Uhuru. Serikali imeonesha nia ya kuwasaidia waimbaji hao kurejea tena kwenye muziki.

Naibu Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Juliana Shonza aliwakutanisha na uongozi wa Wanene Studios waliokubali kuchukua jukumu la kuwarudisha tena kwenye muziki. Tayari wameanza kuingia studio kuandaa kazi mpya katika studio hizo kubwa katika ukanda wa Afrika Mashariki.

Babu Seya na Papii Kocha wamefanya photoshoot kitu ambacho Papii amekiri kuwa ni kigeni mno kwao kutokana na kuwa gerezani kwa miaka 14 na wametoka katika nyakati ambazo muziki wa Tanzania umepiga hatua kubwa ukilinganisha na zamani.

“Miaka 14 si mchezo, mambo kama haya, niliyamiss, nimemiss vitu vingi, picha za ukweli, mambo haya kule tulipotoka hamna. lazima uelewe hii ni dunia nyingine,” -Papii Kocha

Papii pia amesema kuwa kazi zao mpya zitakuwa kali zaidi ya zile za zamani. “Kwasababu tumejipanga vizuri na kazi zinazokuja zitakuwa nzuri zaidi ya zile tulizofanya mwanzo,” – Papii Kocha

VIDEO: JUX AMWAGA MAHELA KWA VANESSA AVUNJA RECORD KWA KUNUNUA CD 25 MLIMANI CITY

Soma na hizi

Tupia Comments