Magazeti

Hizi ni story kubwa tano nilizokuchambulia kutoka kwenye Magazeti ya T’zania leo Jan 03

on

magazetiniMWANANCHI

Mkazi wa Morogoro Andrew Chimulimuli ametangaza kuuza figo yake kwa kwa kiasi cha sh. Mil 90 ili kukabiliana na ugumu wa maisha na kama akitokea mteja akahitaji kupunguziwa gharama watafanya mazungumzo.

Nimeamua kujitolea nafsi yangu ili nisaidie familia yangu kwa sababu mimi si kitu kama sina fedha, ndiyo maana nimejitolea kutoa figo yangu nipate fedha”—Andrew.

Kwa mujibu wa Takwimu za Wizara ya Afya kuna wagonjwa 470,000 T’zania ambao figo zao zimeshindwa kufanya kazi kabisa na wanahitaji upandikizaji.

Mkurugenzi wa taasisi ya Figo Tanzania Jaji Frederick Werema aliwahi kusema kuwa kitendo cha uuzaji wa figo ni kosa la jinai, ili kuuza ni lazima wahusika wafuate taratibu za kisheria.

Uchunguzi wa gazeti la Mwananchi ulionyesha kuwa wapo baadhi ya watu ambao wamekuwa wakiuza figo kiholela.

NIPASHE

Matembezi ya vijana watatu wafuasi wa CHADEMA, Atanasi Michael, Khalid Seleman na Juma Maganga waliotembea kwa muda wa siku 37 kutoka Geita kuelekea Ikulu Dar yameingia nyongo baada ya kuishia mikononi mwa Polisi.

Wafuasi hao walifanya maandamano hayo kulaani matumizi mabaya ya rasilimali za nchi, rushwa, kulinda ufisadi kwa kutokuchukua hatua dhidi ya wahusika na uvunjifu wa haki za binadamu.

Baada ya kufika Ubungo, Polisi waliwaambia waende katika ofisi za za Mkuu wa Wilaya ya K’ndoni ambapo walitii amri hiyo, baada ya kufika waliambiwa hawatoruhusiwa kuendelea mpaka wapate vibali vya kwenda Ikulu ambavyo hawakuwa navyo, wakafanya maamuzi ya kuendelea na safari ya kuelekea Ikulu hatua chache mbele wakakamatwa na Polisi na kuwekwa ndani.

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa CHADEMA, Tumaini Makene alisema walipata taarifa za wafuasi wao sita kuwekwa ndani na Polisi waliwagomea kuwawekea dhamana.

 

MTANZANIA

Ofisa uhusiano wa Taasisi ya MOI, Frank Matua amesema jumla ya wagonjwa nane wametelekezwa katika taasisi hiyo na ndugu zao baada ya kutibiwa na kujikuta hawana kwa kwenda.

Matua amesema kati yao wapo wagonjwa ambao wamekaa kwa zaidi ya miaka miwili, wengine mwaka mmoja na wengine miezi zaidi ya miwili ambao walifikishwa kutibiwa baada ya kupata ajali ya barabarani.

Ofisa huyo amesema wengine wana matatizo ya akili, hawawezi kujieleza hivyo ni ngumu kupata taarifa zao, hawawezi kuwaruhusu wakaondoka na kuzagaa mitaani hivyo wanalazimika kuendelea kuwa nao hapo hospitalini kwa muda wote wakisubiri ndugu zao kujitokeza.

TANZANIA DAIMA

Watu 36 wamefariki na wengine 40 kujeruhiwa wakati wakiwa katika hekaheka za kusherehekea mwaka mpya China ambapo watu hao walipatwa mkasa huo wakati wakigombea kudaka karatasi za kuponi zilizofanana na dola zilizokuwa zikirushwa kutoka ghorofani.

Mtu aliyekuwa akizirusha kuponi hizo ni mmoja ya majeruhi, alihojiwa akasema kuwa alizirusha kama sehemu ya kusherehekea mwaka mpya.

Watu waliozitapa kuponi hizo wanasema hazikuwa kuponi ila ni dola feki, Rais wa China Xi Jinping ametaka uchunguzi ufanyike na watuhumiwa wakamatwe haraka, Polisi walisema hawajabaini kama fedha hizo zilikuwa bandia kwa kuwa zilikuwa zimekanyagwa na watu.

HABARI LEO

Mkurugenzi Mtendaji Wilaya ya Iramba Singida, Halima Mpita amenusurika kifo baada ya kulipukiwa na kitu ambacho kinadhaniwa kuwa bomu la kutengenezwa kienyeji.

Kamanda wa Polisi Singida, Thobias Sidoyeka amethibitisha kutokea kwa tukio hilo nyumbani kwa Mkurugenzi huyo wakati akijiandaa kwenda kazini, mlipuko huo ulitoka kwenye bahasha ambayo aliipokea juzi kutoka kwa Katibu Muhtasi wake.

Ndani ya bahasha hiyo kulikuwa na ujumbe “Poleni sana, hatuwezi kufanya dili la milioni 90 halafu mkala peke yenu, sisi mkatudhulumu tukawaacha”, baada ya kuisoma alienda nayo nyumbani bila kujua kama kuna kitu kingine ndani.

Wakati akijiandaa kwenda kazini siku ya jana ndipo mlipuko huo ulipotokea, hakuna aliyekamatwa ila Polisi wanaendelea na upelelezi wakishirikiana na JWTZ ili kubaini kama mlipuko huo ulitokana na bomu.

Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook

Tupia Comments