Habari za Mastaa

Cardi B atema cheche kwa wale wanaosema hakustahili tuzo ya Grammy(+video)

By

on

Baada ya rapper Cardi B kuvunja rekodi ya kuwa msanii wa kwanza wa kike kuondoka na tuzo ya Album bora ya Hip Hop (Invasion of Privacy) katika tuzo za Grammy zilizofanyika February 10,2019 California nchini Marekani.

Kumekuwa na maneno mengi kwenye mitandao ya kijamii ambapo asilimia kubwa ya watu wameendelea kusema kuwa Cardi B hakustahili kushinda tuzo hizo. Hivyo Cardi B ameonekana kuchoshwa na maneno hayo ambayo yamekuwa yakiendelea na kusema kuwa amejituma sana kuitayarisha Album hiyo.

” Sio style yangu kuwafanya wengine wawe chini na siwashauri wengine kufanya hivyo, nimechoshwa na maneno yenu na nimeona yote ambayo yalikua yakiendelea tokea jana, nimejituma sana kuitayarisha, album yangu imeenda Platinum mara mbili pamoja na kukamata nafasi za juu kwenye kila chati”

“Kuna wakati nilikaa studio miezi mitatu mpaka kufikia nikawa nalala studio hata siku 4 mfululizo sikujua kitanda changu na nilikua mjamzito, tulikua hatulali wala kufanya kitu chochote zaidi ya kuhiangaikia Album imalizike” >>> Cardi B 

EXCLUSIVE: RUCK BABY MWENYE MAVAZI YA UTATA KAZUNGUMZA

Soma na hizi

Tupia Comments