AyoTV

Kuanzia Jumatatu, usishangae kukosa usafiri wa Daladala ukiwa Mwanza

on

Story kubwa ambayo ina make headlines leo June 22, 2017 kutoka Mwanza ni kwamba huenda shughuli za usafiri zikasimama baada ya Chama cha Madereva Daladala kuazimia kufanya mkutano kujadili ushuru na faini wanazotozwa na Askari wa Usalama Barabarani.

Ayo TV na millardayo.com zimekutana na Hassan Dede ambaye ni Mwenyekiti wa Madereva wa Daladala Mwanza:>>>”Hatuko tayari ufanyaji wa kazi wa mazoea. Na sisi tuelimishane maeneo yale hayafai kushusha abiria. Wanaofanya hili hawafikirii kama sisi sio muhimu kwa wananchi. Wangejua kama sisi ni muhimu kwa Wananchi, moja wangesitisha zoezi lao la kuwakamata madereva.

“Gari takribani 20 zipo kituoni pale. Na mimi nimesema yaacheni msiyatoe kituoni yaacheni. Sisi tukae, tuandae barua, tutakwenda huko Mahakamani watuambie Mwanza vituo viko wapi. Kama wamekamata gari Ishirini ziko pale wanataka Elfu Thelathini inasaidia nini?

“Magari mengine ni ya kwao, ni ya Polisi lakini yale ya kwao hawayakamati na yakikamatwa yanaachiwa. Ya kwetu sisi, walalahoi sisi tunakamatwa. Inawekwa gari Uani kule mpaka ulipe Elfu Thalathini.

“Nimekuwa Kiongozi tangu 2009 mpaka leo tumekuwa tunapigia kelele vituo. Mpaka leo vituo hakuna ambacho tumeteweza kutengenezewa mpaka 2017 leo. 2009 mpaka 2017 leo mwezi wa Sita hakuna kituo” – Hassan Dede.

“Hakuna mwenye mimba atakayerudi shuleni” – Rais Magufuli

Soma na hizi

Tupia Comments