AyoTV

Rais mwingine aliyealikwa na Rais JPM kutembelea Tanzania

on

Rais Abdel Fattah el-Sisi wa Misri anatarajia kutembelea Tanzania baada ya kualikwa na Rais Magufuli ikiwa ni moja ya mikakati ya kuimarisha mahusiano ya kidiplomasia na kufungua milango ya fursa za kiuchumi baina ya nchi hizo.

Akieleza ujio huo Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Uhusiano wa Afrika Mashariki Dr. Aziz Mlima amesema kwa miaka mingi nchi hizi mbili zimekuwa na mahusiano katika maeneo mbalimbali kama kilimo, maji pamoja na elimu.

>>>”Misri pia imefanya uwekezaji nchini Tanzania ambapo kwa sasa yapo makampuni manane ya Wamisri ambayo gharama zake zinafika dola Milioni 800 ambazo zimetoa jumla ya ajira 957 kwa Watanzania. Hii inaonesha kwa jinsi gani Tanzania inanufaika na mahusiano haya.” – Dr. Mlima.

ULIPITWA? Press ya kwanza ya Paul Makonda baada ya kumalizana na Wahariri…tazama hapa kwenye video hii!!

Soma na hizi

Tupia Comments