Mimba, utoro na vifo vimetajwa kuwa ni miongoni mwa changamoto kubwa ambazo mtoto wa kike anakumbana nazo katika safari yake ya kimasomo ambapo wengi wmekuwa wakishindwa katika bila kufikia malengo yao licha ya serikali kujitahidi kuwakwamua.
Mkurugenzi Mtendaji HakiElimu John Kalage amebainisha kuwa licha ya watoto wa kike kuandikishwa shule kwa uwiano sawa na watoto wa kiume lakini wanashindwa kufikia malengo kwa sababu ya changamoto.
>>>”Kuna changamoto nyingi sana ambazo watoto wa kike wanakumbana nazo ambazo zinafanya waache shule. Kwa mfano, katika Takwimu za elimu za mwaka jana Basic Education Statistics ambazo zilikuwa zinatoa taarifa ya mwaka 2015, kuna watoto wa kike takribani 69,067 ambao waliacha shule kwa sababu mbalimbali ikiwemo mimba, ikiwemo utoro, ikiwemo vifo.
“Tukiangalia, tunaona kwamba katika jitihada ambazo serikali imefanya pamoja na wadau mbalimbali kuhakikisha kwamba kunakuwa na fursa sawa au uwiano wa kijinsia imeonekana kwamba katika uandikishaji watoto wa kika na wa kiume wanaandikishwa sawa Shule za Msingi.
“Unapokwenda juu, pale katika udahili uwiano ni moja kwa moja lakini unapokwenda pale juu unaona kwamba idadi ya watoto wa kike inakwenda ikipungua.” – John Kalage.
ULIPITWA? Polisi DSM wazungumzia tukio la Walemavu kupigwa mabomu. Kwenye hii VIDEO kuna kila kitu Jeshi la Polisi imesema kuhusu tukio hilo. Bonyeza PLAY kutazama!!