Top Stories

Dakika 7 za kilichosemwa CHADEMA mbele ya Waandishi wa habari.

on

mics chademaChama cha demokrasia na maendeleo {CHADEMA} kimesema Bunge maalumu la katiba na vikao vyake vinavyoendelea hivi sasa havina uhalali wa kukubalika kwa sababu hakuna maridhiano wala muafaka wa kitaifa hivyo limepoteza uhalali wake kwa sababu ya kuvunjwa kwa sheria ambapo pia chama hiki kimemtuhumu Mwenyekiti Samweli Sitta kuwa analiongoza bunge hilo kuvunja sheria.

Aliyeyazungumza haya ni naibu katibu mkuu wa Chadema John Mnyika ambae pia ni mbunge wa Ubungo na kuongeza kwamba kilichofanywa juzi na bunge ni kitendo kisichovumilika kwa kuvunja sheria maalumu ya bunge kwa kuruhusu upigwaji wa kura kwa mtu akiwa nje ya bunge.

Kabla ya kumsikiliza kwa mapana hapa chini, nataka nikupe baadhi ya mistari iliyoandikwa na baadhi ya Magazeti ya Tanzania September 23 2014 >>>> #MWANANCHI – Bunge kutuma Ofisa Saudi Arabia kusimamia kura #TanzaniaDAIMA – UKAWA waokoa shilingi bilioni 2.3, ni kutokana na kususia bunge, katibu akiri hazijaombwa Serikalini.

Karibu kwenye familia ya millardayo.com na uzipokee stori zote kwa kutumiwa usiku au mchana baada tu ya kujiunga kwa kubonyeza hapa mtu wangu >>> Twitter Instagram Facebook

Tupia Comments