Premier Bet SwahiliFlix Ad Tigo Ad

Top Stories

Picha 3 za jinsi Waziri mkuu wa Uganda alivyonyang’anywa ulinzi nyumbani baada ya kutimuliwa kazi.

on

ug1Jana ndio Waziri mkuu mpya wa Uganda Ruhakana Rugunda kaapishwa ila kabla yake alikua ni Amama Mbabazi ambae alifutwa kazi wiki kadhaa zilizopita baada ya kukaa madarakani toka May 2011 akitokea kwenye Uwaziri wa Ulinzi.

September 18 2014 ndio Rais Museveni alimuandikia Spika wa bunge barua kumuarifu kuwa ameamua kumuondoa waziri mkuu huyo na nafasi yake kuchukuliwa na aliyekua Waziri wa Afya ambae kwa sasa ana umri wa miaka 67.

ug2Kwa mujibu wa ripota wa TZA (millardayo.com na AyoTV) waziri huyu alietimuliwa alikua Waziri mkuu wa nne toka Rais Museveni aanze kuitawala nchi hiyo January 1986 ambapo mpaka sasa amewahi kuwa na Makamu wa Rais wanaofikia wanne.

Picha zote hizi zinaonyesha wakati Serikali ya Uganda ilipomnyang’anya ulinzi wa Wanajeshi waziri huyu mkuu baada ya kufutwa kazi ambapo kwenye hii picha ya chini anaeonekana ni mke wake akilalamika kwa kutoamini kilichotokea kwani mume wake na Rais Museveni wamekua marafiki wakubwa.

Vyombo mbalimbali vya habari vimeripoti kwamba kuna mambo mengi yaliyosababisha kufutwa kazi kwa waziri huyu mkuu lakini mambo hayo hayajawekwa wazi.

ug3

Nyuma hii unayoiona ni nyumba anayoishi na inayomilikiwa na Waziri huyu mkuu aliefutwa kazi.

Unataka niwe nakusogezea kila stori inayonifikia zikiwemo pichaz, video’s na stori zenyewe? niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook cha kufanya ni kujiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook

Tupia Comments