AyoTV

Jibu alilolitoa Jay Z akitembea baada ya kumsikia mtu wa pembeni akiuliza Jay Z ni nani? (video)

on

JayRapper Jay Z na mke wake wapo Paris Ufaransa wiki hii ambapo wakati Jay akiwa kwenye matembezi huku akiwa amembeba mtoto wake ilitokea mmoja wa Watalii baada ya kumuona Jay akauliza ‘huyu ni nani? unajua jibu alilotoa mume huyu wa Beyonce?

Kabla ya Jay Z kujibu, mlinzi wake aliekua ametangulia mbele hatua chache huku Jay akifata kwa nyuma na timu yake alikua akizuia watu kupiga video ambapo huyu mtalii alikua akipiga video, akawa anashangaa imekuaje akatazwe kupiga video… swali lililoambatana na kuuliza huyu anaepita nani? Jay Z kwa kiburi na yeye akamjibu kwa kuuliza ‘wewe ni nani?

JAY 2Japo inaonekana Jay Z alijibu kwa dharau, wataalamu wa mambo wanasema huenda kweli mtalii huyu hakuwa anajua anaepita ni nani manake alikua kwenye eneo la kitalii ambalo wengi wanaokuwepo hapo huchukua kumbukumbu kupitia camera zao.

Unataka stori kama hizi zisikupite? unataka kuwa kupata kila kinachonifikia? karibu ujiunge na mimi kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Instagram Facebook

Tupia Comments