Habari za Mastaa

Uliipata hii ya Rose Muhando? inaitwa jiwe….

on

Rose Muhando 1Ni mamilioni ya Watanzania wanaguswa na kipaji cha mwimbaji Rose Muhando na ndio maana wamemfanya kuvunja rekodi za mara kwa mara kwenye mauzo ya nyimbo zake dukani na hata kwenye matamasha anayokwenda.

Rose Muhando ambae makazi yake ni Dodoma, amekua na mfululizo wa kutoa kazi zake chini ya mkataba na kampuni kubwa ya Sony na sasa kaiachia single yake ya pili chini ya studio za Sony Music Africa ambapo kama unakumbuka single yake ya kwanza ni ‘Wololo’ kwenye hii album ya Yesu Kung’uta chini ya usimamizi wa Rock star 4000 ambazo zote hizi zimepatikana kupitia mkito.com

mkito.com ni mtandao ambao ni mwepesi kuingia na kuutumia kama vile kudownload au kusikiliza wimbo wowote uliopo lakini vilevile ni website ambayo inasaidia kunyanyua vipato vya Wasanii kwa kupata malipo kila nyimbo zao zinaposikilizwa au kuwa downloaded hivyo karibu umuunge mkono msanii wako kwa kubonyeza >>>> HAPA

Tupia Comments