Habari za Mastaa

Suge Knight hataki tena kusikia kuhusu ishu ya kupigwa risasi?

on

Askari wanaohusika na kesi ya Suge Knight kupigwa risasi August mwaka huu wanasema wamemfahamu mtu aliyefanya kitendo hicho lakini hawana ushahidi wa kutosha ili kuweza kumkamata.

Mtandao wa TMZ wa Marekani umesema baada ya askari wa Los Angeles kuangalia kamera na kukusanya taarifa mbalimbali kutoka kwa mashahidi wamempata muhusika aliyempiga risasi Suge na wanaendelea kukusanya mashahidi ili kupata maelezo zaidi juu ya kesi hiyo.

suge 1

Suge Knight alipigwa risasi mara sita kwenye klabu iitwayo West Hollywood 1Oak kwenye party iliyoandaliwa na kufanyika kabla ya utoaji wa tuzo (VMAs) ambayo iliendeshwa na mwimbaji staa Chris Brown.chris

Muhusika mkuu huyo wa zamani wa studio iitwayo Death Rows alisema hausiki tena na kitendo hicho kilichotokea cha kupigwa risasi >>>  ‘Mimi sijui kinachoendelea, na hata kama najua nani alishika risasi sidhani kama kuna umuhimu, ninaendelea vizuri na nina furaha kuwa naendelea vizuri, kilichotokea kimeshatokea’Suge

Tupia Comments