Habari za Mastaa

Tutarajie video mpya ya @VanessaMdee kutoka nje ya Tanzania?

on

V 1Maoni ya Wasanii wengi wakubwa wa Tanzania niliozungumza nao kwa asilimia kubwa hayapingani na maamuzi ya mastaa wengi wa bongo kwenda kufanya video za muziki wao nje ya Tanzania na hii ni sababu ya kuutafuta ubora wa kuiuza vizuri bidhaa yao.

Miongoni mwa wasanii waliozungumza na Fid Q ambae anasema kwa kutolea mfano mdogo kwamba Tanzania ina warembo wazuri sana wa kutokea kwenye video lakini huwa hawakubali sababu wanaona ni kujishushia hadhi, kingine ni Madirector kutaka kufanya wanavyojua wao na hawawapi Wasanii nafasi ya kueleza wanatakaje.

Baada ya kukupa hayo, taarifa ikufikie kwamba mwimbaji staa wa hit single ya ‘hawajui‘ Vanessa Mdee amesafiri kwenda nje ya Tanzania kwa ajili ya kufanya video ya hiyo single ambapo aliiweka hiyo picha hapo juu kwenye instagram yake na kuandika hii caption hapa chini akiwa uwanja wa ndege Dar es salaam.
V 2Kaenda nchi gani? anaifanya na nani? mengine ya ziada unataka kuyajua? kaa karibu na millardayo.com mtu wangu pia jiunge na mimi kwenye twitter, facebook na instagram ili kikitokea chochote tu nikudondoshee.

Tupia Comments