AyoTV

Kwa hiyo Ray J katoa ushauri kwa Tyga baada ya kusemekana kutoka na Kylie wa Kardashian?

on

Tyga 1Ni kwenye zile stori za mastaa mbazo huwa haziishi yani ambapo kwenye hii post amekabidhiwa mwimbaji Ray J baada ya kuzungumza na kusema kwa mtazamo wake yeye ni vyema rapper Tyga akarudiana na mpenzi wake aitwae Blac Chyna kuliko kuingia kwenye uhusiano wa kimapenzi na Kylie Jenner ambae ni mrembo kutoka familia ya kina Kim Kardashian.

Tukumbuke kwamba Ray J alishawahi kuwa mapenzini na Kim K kwa muda mrefu ambapo mapenzi yao yaliingia kwenye headlines kubwa kutokana na mkanda wa video uliorekodiwa wawili hawa wakiwa mahabani.

Ray J ambae ameonyesha kwamba anaijua vizuri familia ya Kardashians amesema Tyga arudi kwa Blac Chyna ambae wamezaa mtoto mmoja lasivyo kwenda kwa Kylie ni kuvuka mipaka.

Tyga 2

Tyga na Blac Chyna.

tyga 3

Tupia Comments