Premier Bet
TMDA Ad

Habari za Mastaa

Ni Cardi B tena kaweka rekodi Billboard Hot 100

on

Female Rapper Cardi B kutokea Marekani ameingia kwenye headlines baada ya kuvunja rekodi kwa kuwa rapa wa kwanza wa kike kushika namba moja kwenye chart za Billboard Hot 100 na wimbo wake wa “I Like it” akiwa amemshirikisha Bad Bunny pamoja na J Balvin.

Ngoma hiyo inapatikana kwenye album ya Cardi B Invasion of Privacy ikiwa wimbo huo ulitoka April 2018 na huu ni wimbo wake wa pili kushika nafasi katika chart za Billboard Hot 100 ikiwa pia wimbo wa Bodak Yellow uliwahi kushika namba moja mwezi October 2017 .

Hivyo ngoma hizo mbili kuingia kwenye Billboard Hot 100 na kushika nafasi ya kwanza zinamfanya Cardi B kuwa msanii wa kwanza wa kike  kwenye genre zote na kuwafunika Lil Kim, Iggy Azalea, Shawanna ambao waliwahi pia kuongoza katika chart hizo mara moja tu.

Ahadi ya Roma Mkatoliki kama Mexico atamfunga Brazil leo

 

Soma na hizi

Tupia Comments