Michezo

Lebron James kaandika ujumbe kufuatia kifo cha rafiki yake Kobe Bryant

on

NI Healdines za msiba mzito kwenye tasnia ya mpira wa kikapu duniani mnamo tarehe 26 baada ya mkongwe Kobe Bryant kufariki kwa ajali ya helkopta akiwa na binti yake wa miaka 13 Gigi na wengine 7

Msiba huu umepokelewa kwa hisia tofauti sana na wachezaji pamoja na wadau mbalimbali wa michezo duniani,sasa hapa nina ujumbe wa Lebron James ambae alikuwa rafiki wa marehemu Kobe Bryant

NUKUU

Siko tayari lakini kama binadamu nimekaa hapa nikijaribu kuandika kitu kwaajili ya hii habari lakini kila wakati ninapojaribu ninaanza kulia tena nikikufikiria wewe, mpwa Gigi na urafiki, undugu tuliokuwa nao’– Lebron James

Nitaendeleza urithi wako, una umuhimu sana kwetu sote hapa hususani #lakersnation na ni jukumu langu kuiweka rekodi yako mgongo na kuifanya iendele, tafadhali nipe nguvu kutoka mbinguni na unitazame’- Lebron James

 

 

Soma na hizi

Tupia Comments