Leo May 28,2018 imetimia miaka mitano tokea Tanzania ipokee taarifa ya kifo cha mkali wa Bongo Fleva Marehemu Albert Kenneth Mangwair ambaye umauti ulimkuta Johannesburg Afrika Kusini May 28,2013 na kuacha pengo kubwa katika muziki wa Bongo Fleva
Marehemu Albert Mangwair alianza kazi ya muziki mwaka 2003 baada ya kukutana na mtayarishaji mahiri wa muziki P Funk Majani na kuanza naye kazi rasmi na kuachia ngoma yake ya kwanza “Ghetto Langu” ambayo ilimfungulia milango ya maisha yake katika muziki na kumpatia umaarufu mkubwa Tanzania.
Marehemu Albert Mangwair aliwahi kufanya kazi na mastaa mbalimbali akiwemo Fid Q, Mr Blue, Darkmaster, Chid Benz, TID na wengine wengi hivyo Marehemu alifariki akiwa na umri wa miaka 31 (November 16, 1982-May 28,2013) na kuacha pengo ambalo alitozibika kutokana kuacha ngoma kali zilizopendwa na watu mbalimbali hadi sasa, “Pumzika kwa Amani Ngwair”.
Ruby kazungumza baada ya kuimba wimbo wa Nandy