Mix

FULL VIDEO: Alichokizungumza Wema Sepetu nyumbani kwa Godbless Lema

By

on

Leo March 5, 2017 Muigizaji Wema Sepetu amefika nyumbani kwa Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema ambaye ameachiwa kwa dhamana kutoka mahabusu siku mbili zilizopita. Wema alikwenda kumjulia hali Mbunge huyu na kuzungumza naye baada ya kujiunga na CHADEMA wiki chache zilizopita.

Kati ya vitu Wema Sepetu amevizungumza ni pamoja na kusema kuwa ameshaamua kuingia moja kwa moja kwenye chama hicho cha upinza na hana mpango wa kuondoka, pia suala la mama yake kukamatwa baada ya kudaiwa kuchukua pesa kwaajili ya kumuuzia nyumba mfanyabiashara Alex Msama.

Kingine ni suala la gari alilopanda kutoka Kenya kumatwa mpakani wakati akiingia Arusha March 4, 2017 huku wakaguzi wakisema gari alilokuwepo Wema halifanani na taarifa walizonazo kwenye mifumo yao ya kumbukumbu.

Nimekuwekea hapa FULL VIDEO bonyeza Play kutazama kila kitu Wema Sepetu amekiongea 

VIDEO: Kauli ya CHADEMA baada ya Wema Sepetu kujiunga na chama hicho, Tazama hapa chini.

Soma na hizi

Tupia Comments