Michezo

Zlatan Ibrahimovic kataja sababu ya kumkatalia Wenger kujiunga na Arsenal

on

Mshambualiaji wa zamani wa club ya Man United anayecheza LA Galaxy ya Marekani kwa sasa Zlatan Ibrahimovic ni miongoni ya wachezaji soka wanaojiamini sana ndani na nje ya uwanja, hiyo ni baada ya leo kuweka wazi kuwa aliwahi kuombwa kwenda kuomba kufanya majaribio Arsenal akataa.

Zlatan Ibrahimovic ameweka wazi kuwa aliwahi kocha wa zamani wa Arsenal Arsene Wenger aliwahi kumuhitaji kwenda Arsenal ila aligoma baada ya kocha huyo kumtaka aende kwanza akafanye majaribio kabla ya kusaini mkataba, kitu ambacho Zlatan anaamini hakuwa mchezaji wa kujaribiwa.

“Nilipokuwa na miaka 17 Arsene Wenger alinitaka niende Arsenal nikafanye majaribio, nilikataa kwa sababu mimi huwa sifanyi majaribio”>>>> Zlatan Ibrahimović

Rais Karia kaiomba kamati ya RC Paul Makonda kuhamishia nguvu kwa Serengeti Boys

Soma na hizi

Tupia Comments