Top Stories

Mtoto afariki akiombewa na Mchungaji… Ilikuwaje?

on

Leo June 8, 2018 Nakusogezea stori kumhusu Mtoto ambaye ni mgonjwa ambapo amefariki baada ya wazazi wake kumpeleka kuombewa na Mchungaji wa kanisa la ‘Kanitha Ya Ngai’ ambaye haruhusu waumini wake kutumia tiba za kisasa.

Wazazi hao kwa sasa wamekamatwa na Polisi katika kijiji cha Kinungi kaunti ya Nakuru nchini Kenya huku Mchungaji huyo akitokomea kusikojulikana.

Katika eneo la Kinungi kunatajwa kuwa na waumini wengi wa kanisa hilo ambao hawaamini katika tiba za kisasa.

Mzazi wa kwanza kukamatwa alikuwa ni mzazi wa kike ambaye alikamatwa baada ya kwenda kuomba kibali cha kumzika mtoto wake kwa Chifu wa eneo hilo.

Kwa mujibu wa Chifu, visa vingi vya waumini hao vimeongezeka sana kwa siku za hivi karibuni na amesema kuwa kwa sasa wanamtafuta mchungaji huyo ambaye amekimbia baada ya kusikia anatafutwa ili ahojiwe.

Tazama LIVE mapya aliyoibuka nayo Dr. Shika akizungumza na Waandishi ‘Tutaelewana’

VIDEO: Ulivyopokelewa mwili wa ‘Sam wa Ukweli’, Mastaa waliohudhuria

Soma na hizi

Tupia Comments