Ajali

Mambo 6 kuhusu Majeruhi ajali ya Wanafunzi Arusha waliofatwa na Ndege kupelekwa Marekani

on

Ajali ya basi dogo la Wanafunzi Karatu Arusha iliua 32 weekend iliyopita na kuacha Majeruhi watatu ambao wamekua wakitibiwa kwenye Hospitali ya mkoa wa Arusha, Mount Meru.

Mbunge wa Singida kaskazini Lazaro Nyalandu amekua mstari wa mbele kuhakikisha watoto hawa wamesaidiwa kimatibabu pamoja na kisaikolojia ambapo juzi May 11 aliongea na AyoTV na millardayo.com Arusha.

1. ‘Ninapenda kutangaza kwa furaha kubwa sana kwamba tumefanikiwa kupata Ndege kubwa inayoweza kutumika kama ‘AMBULANCE‘ angani na inaondoka North Carolina Marekani kuja moja kwa moja Kilimanjaro Tanzania kuwachukua hawa majeruhi’ – Nyalandu

2. Baada ya taarifa hizo, Ndege hiyo ya Samaritan Purse DC 8 N782SP imewasili Kilimanjaro     Tanzania leo May 13 2017 ikiwa na Marubani wanne na Wahudumu wake 7  tayari kuwabeba Majeruhi hao ambao wataambatana na wazazi wao mpaka Marekani kwenye matibabu.

Mmoja wa Marubani wa Ndege hiyo akiwa na Mbunge Lazaro Nyalandu kwenye uwanja wa Ndege KIA.

Rubani wa Ndege hiyo amewaambia Waandishi kwenye uwanja wa ndege Kilimanjaro (KIA) kwamba wataondoka kesho na watasimama Cape Verde kuweka mafuta na kisha kuelekea Marekani moja kwa moja na wanatarajia kuingia kesho yake usiku.

Tayari Wazazi wa watoto hao watatu wameshapata VISA za kuingia Marekani pamoja na watoto wao na wako tayari kwa safari.

3. Ndege hii imetolewa na shirika la SAMARITAN’S PURSE (mfuko wa Msamaria) linalosimamiwa na mtoto wa Mwinjilisti mkubwa wa Marekani Franklin Graham, familia yao baada ya kupelekewa habari za kilichotokea kwenye ajali ya Karatu walikubali kuituma ndege hiyo kutoka Marekani kuja kuwachukua Majeruhi Tanzania.

Mwinjilisti Franklin Graham

4. Kwenye Ndege hiyo kuelekea Marekani itawabeba Mama wa watoto hao watatu, itawabeba pia Nesi mmoja na Daktari mmoja wa Kitanzania ambao wataendelea kuwahudumia watoto hao ndani ya ndege hiyo yenye uwezo wa kutoa huduma kama Ambulance pia.

5. Ndege hiyo ikishatua North Carolina, SAMARITAN’S PURSE wameandaa Ndege nyingine ambayo pia inaweza kufanya kazi kama AMBULANCE angani iitwayo AIR AMBULANCE na kuwachukua hadi jimbo la Iowa ambako Hospitali ya Mercy imekubali kuwatibu Wagonjwa hawa bure kwa muda wote watakaohitaji matibabu.

6. ‘Tukiwa Marekani tutakua na haki ya kuangalia kinachoendelea ambapo Watanzania na marafiki wa Tanzania wataopenda kuchangia kwa M-PESA na njia nyingine wataruhusiwa, tayari shule 3 za Arusha Braeburn Internation, St. Costantine na International School of Moshi zimejiunga kuandaa mfuko ambao utatumika kuwachangia’ – NYALANDU

Hutaki kupitwa na habari yoyote? Reporter wako MILLARD AYO usiku na mchana yuko tayari kukusogezea zote habari, BREAKING NEWS, picha na video za mastaa… jiunge nae kwenye FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM, SNAPCHAT, YOUTUBE, APP kwenye ANDROID na IOS kote huko kwa jina hilohilo la ‘millardayo’ 

VIDEO: Vilio, huzuni…. miili 32 ya ajali ya Wanafunzi Arusha ikiagwa, tazama kwenye hii video hapa chini

VIDEO: Ajali ya Treni Tanzania, ilikua ikitokea Kigoma- DSM… play hapa chini kutazama

Soma na hizi

Tupia Comments