Michezo

Mohamed Salah amerudi tena, ukame wa mabao fyekelea mbali

on

Usiku wa April 5 2019 club ya Liverpool ya England iliendeleza harakati zake za kupambani Kombe la Ligi Kuu England kwa kucheza dhidi ya Southampton, Liverpool walikuwa ugenini katika mchezo huu na presha ilikuwepo kutokana kuwa na utofauti mdogo sana kati yao na Man City wanaoongoza Ligi timu hizo mbili zinapocheza mchezo wake wa Ligi na wapinzania tofauti zinauona kama fainali.

Liverpool iliingia uwanjani na staa wao Mohamed Salah akiwa kacheza mechi 9 mfululizo pasipo kufunga goli kiasi cha wengi kutabiri kuwa ndio kamaliza msimu, bahati ilikuwa kwa Liverpool ambao walipamba na kufanikiwa kupata ushindi wa magoli 3-1, magoli ya Liverpool yakifungwa na Keita dakika ya 36, Mohamed Salah dakika ya 80 na Henderson dakika ya 86.

Southampto goli lao la mapema dakika ya 9 lililofungwa na Long halikuwasaidia na kuambulia kuona point tatu zikienda Liverpool, baada ya Mohamed Salah kufunga goli la leo anavunja rekodi yake ya kucheza mechi 9 mfululizo bila kufunga goli lolote, hivyo unaweza kusema Mohamed Salah kwa sasa amemaliza ukame wa magoli.

Ukimuuliza Mwinyi Zahera ishu za Ajib kurudi Simba SC….

Soma na hizi

Tupia Comments