Michezo

AUDIO: Taarifa kutoka Mbeya City kuhusu zile stori za Ngassa kuondoka mwisho wa msimu

on

Weekend zilienea stori za Mrisho Ngassa anayeichezea Mbeya City ya Mbeya kuwa ataihama timu hiyo mwisho wa msimu na kurejea Oman kitendo ambacho kimezua maswali mengi kufuatia kuenea kwa taarifa, wote tunajua Ngassa amesaini mkataba wa mwaka mmoja lakini kwanini iliripotiwe kuwa ataondoka mwisho wa msimu ikiwa mkataba wake utakuwa bado haujaisha.

Mbeya City hawamuhitaji tena au wanampango wa kumuuza, millardayo.com imempata katika exclusive interview afisa habari wa Mbeya City Dismas Ten “Kitu pekee ambacho naweza kusema kwa sasa ni kwamba Ngassa ni mchezaji bado wa Mbeya Cityalijiunga na Mbeya City dirisha dogo na alisaini mkataba wa mwaka mmoja”

Kama utakuwa unakumbuka vizuri usiku wa December 15 2016 siku ya mwisho ya kufungwa dirisha dogo la usajili la Ligi Kuu Tanzania bara msimu wa 2016/2017, Mbeya City walitangaza kumsajili Mrisho Ngassa kwa mkataba wa mwaka mmoja akitokea timu ya Fanja FC ya Oman.

VIDEO: ALL GOALS: Simba vs Yanga February 25 2017, Full Time 2-1

Soma na hizi

Tupia Comments