Habari za Mastaa

Kifo cha Sharo Milionea bado kinamtesa Kitale, kaandika haya maneno na kuweka hii picha

on

Screen Shot 2014-11-12 at 2.48.15 AMMwezi November ndio mwezi ambao Tanzania ilipata msiba mwingine hauwezi kusahaulika kwenye kitabu cha kumbukumbu za Wasanii waliotangulia mbele ya haki.

Wakati huu ambapo msanii/mwigizaji marehemu Sharo Milionea anatimiza miaka miwili toka afariki, mmoja wa marafiki zake ambae ni mchekeshaji/Mwigizaji Kitale ameshindwa kuizuia huzuni yake baada ya kukumbuka kifo cha Sharo Milionea.

Kitale aliandika ‘Huu mwezi Huwa unanisumbuaga sanaaa kiukweli karibia mwezi mzima lakini hasa hizi tarehe 24 tarehe 26 na tarehe 28 siku ambayo tuliachana pale Sinza mm nikaenda #IRINGA tarehe 24 kwa ajili ya Show ya marehemu #SAJUKI, tarehe 26 siku ambayo ndio tunarudi kutoka IRINGA ambayo ndio siku marehemu SHARO MILIONEA alipata ajali ya gari, na tarehe 28 siku ambayo alizikwa hizo tarehe kwakeli.!!!

Screen Shot 2014-11-12 at 2.27.25 AM

Hii ndio picha kaiweka baada ya hayo maneno

‘Mungu ndio anajua zimepishana siku mbili mbili 24.26.28 hiyo ndio kazi ya mwenyezimungu na si binadam mbele yake nyuma yetu #R.I.P SHARO MILIONEA mungu ampe kauli dhabiti mdogo wangu tuseme inshaallah.!!!!’

Hayo ndio aliyoyaandika mwigizaji Kitale kuhusu rafiki yake marehemu Sharo Milionea ambae alifariki kwa kupata ajali kwenye hili eneo hapa chini linaloonekana kwenye video.

Tupia Comments