Michezo

Louis van Gaal kayatoa ya moyoni…. anataka nani ashinde Ballon d’Or 2014? Ronaldo na Messi je?

on

Screen Shot 2014-11-20 at 3.53.45 AMWanaowania tuzo ya Ballon d’Or 2014 walishatangazwa ambapo list hiyo pia inawahusisha mastaa wa soka kama Cristiano Ronaldo na Lionel Messi, huku list hiyo ikiwa pia na wachezaji wa Ujerumani iliyoshinda kombe la dunia mwaka 2014 nchini Brazil.

Baada ya ushindi wa Ronaldo na Messi kuchukua headlines sana kocha wa Manchester United Louis van Gaal (63) ameamua kuyatoa ya moyoni na kusema mwaka huu Ronaldo na Messi hawatakiwi kuchukua hiyo tuzo bali ni halali ikachukuliwa na mchezaji wa Ujerumani.

Wajerumani wanaowania tuzo hiyo ni Mario Gotze, Toni Kroos, Philipp Lahm, Thomas Muller, Manuel Neuer na Bastian Schweinsteiger.

Screen Shot 2014-11-20 at 4.04.25 AMAnasema ‘Naamini Ujerumani inafaa kuchukua hii tuzo, mara nyingi imekua tu ni wachezaji maarufu/wanaofahamika ndio wanashinda hii tuzo, kitu kikubwa kushinda ni kombe la dunia ndio maana naamini itachukuliwa na mchezaji wa Ujerumani sababu kiukweli wanastahili

Screen Shot 2014-11-20 at 3.50.45 AMUmeonaje mawazo ya Van Gaal? ungependa nani ashinde Ballon d’Or ya 2014 mtu wangu? naomba niachie maoni yako kwenye comment hapa chini.

Tupia Comments