Habari za Mastaa

Zile stori za Instagram!! hapa Wema hapa Diamond Platnumz kwenye siku moja Kampala

on

InstaPamoja na kuwepo kwa taarifa ambazo mwenyewe Diamond Platnumz ameshindwa kuthibitisha kuhusiana na kuwa na uhusiano na staa wa Uganda aitwae Zari, mastaa hawa wameonekana kuwa karibu zaidi na kuendelea kufanya kazi kwa pamoja huku wakiendelea kutawala vyombo mbalimbali vya habari kwa kile kinachodaiwa kuwa wako kwenye ‘project

Hizo stori hapo juu zinaambatana na stori nyingine kwamba Diamond na Wema wameachana hivyo kwa sasa Diamond anatajwa kuwa na Zari.

Wema na Diamond wamechukua tena headlines leo kwenye Instagram ambapo wote wamejikuta wakiwa wanapromote events mbili tofauti zitazofanyika siku moja ndani ya jiji la Kampala.

Diamond aliweka picha hii hapa chini na kuandika kumsupport Zari kwenye event atakayoifanya December 18 2014 Kampala Uganda >>> kama mlivyokuwa kimya wakati nasupport watu wengine… Muendelee hivyohivyo…Hasa niwaskie kwenye hii #AllWhiteParty 18th Dec 2014 at Guvnor night club in Kampala UG Usikose!… @zarithebosslady’ ambapo wakati Diamond akiyaandika hayo Wema nae kwenye insta yake aliandika kuipigia debe event ya mwimbaji Jose Chameleone ambayo inafanyika siku hiyohiyo ya Dec 18 Kampala >>> Hatari….!!!! Hatari….!!!! Hatari….!!!!! Sijawahi kufika Uganda lakini kwa hii ntapanda ndege kabisa kwenda kumsupport my brother @jchameleone @jchameleone @jchameleone @jchameleone @jchameleone @jchameleone …. Basi tutakutana pale kati tar 18 kwenye hio show ya kufunga mwaka… Ama nene….

Zari 1

zari 2

zari 3

zari 4Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook

Tupia Comments