AyoTV

EXCLUSIVE: Miss Tanzania afunguka baada ya kutoka Miss World, azungumzia alichokipata

on

Tunayo Exclusive story kutokea kwa Miss Tanzania, QueenElizabeth Makune ambapo amezungumza kwa mara ya kwanza tangu aliposhindwa kunyakua taji la Miss World, mashindano ambayo yamefanyika nchini China.

QueenElizabeth amesema anawashukuru Watanzania kwa mchango wao, pia amejifunza mengi nchini China na anashukuru kwa matokeo aliyoyapata.

“Nimejifunza vitu vingi sana ikiwemo tamaduni, vimenijenga mimi kama mrembo na safari yangu haijaishia hapo huu ni mwanzo tu,”amesema.

Katika mashindano hayo ya Miss World yaliyofanyika December 8, 2018 Sanya nchini China, mrembo kutokea Mexico Vanessa Ponce de Leon ndiye aliyetawazwa kuwa Miss World.

VIDEO: Miss Tanzania alivyopokelewa uwanja wa ndege DSM

Soma na hizi

Tupia Comments