Stori Kubwa

Alichokisema Balozi wa Marekani kuhusu filamu ya wanaoishi na UKIMWI

on

Kaimu Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Dk,Inmi Patterson amezungumzia filamu ya Kitanzania iliyotambuliwa na matamasha makubwa ya filamu duniani inayohusu kuwatetea watu wanaoishi na Ukimwi.
Akizungumzia filamu hiyo, Dk.Patterson amesema filamu hiyo imetengezwa na vijana wa Kitanzania ikiwa imebeba maudhui ya kuwatetea watu wanaoishi na Ukimwi Tanzania, ambapo waigizaji wake wengi ni wale ambao hawajapitia mafunzo rasmi.
Amesema filamu hiyo imeaonyeshwa kwa mara ya kwanza jijini London wiki chache zilizopita ambapo Matamasha makubwa ya filamu yameitambua filamu hiyo.
“Kama sehemu ya maadhimisho ya miaka 15 ya Mfuko wa Rais wa Marekani wa Kupambana na Ukimwi, Ubalozi wa Marekani unashirikiana na Baraza la taifa la Ukimwi kwa ajili ya kuionesha filamu hii katika mikoa mbalimbali,”amesmea Dk.Patterson.
BREAKING: MBOWE APELEKWA DUBAI KIMATIBABU, WENZAKE WASOMEWA MAELEZO YA AWALI

Soma na hizi

Tupia Comments