Bodi ya Nyama Tanzania imesema Tanzania ina mifugo mingi katika nchi za Afrika ambapo yenyewe ni ya pili, lakini bado ulaji wa nyama upo chini ambapo kulingana na viwango vya FAO mtu anatakiwa kula Kilo 50 kwa mwaka, ambapo kwa Tanzania watu wanakula Kilo 15 kwa mwaka.
Kaimu Msajili wa Bodi ya Nyama Tanzania, Iman Sichalwe amesema kwa sasa hali ya mifugo nchini Tanzania ina mifugo mingi ukilinganisha Ethiopia na Sudan, ambapo makadirio ya Ng’ombe ni milioni 30.5, Mbuzi Milioni 18.8, Kondoo Milioni 5.3 Kuku wa asili ni Milioni 38.2 na kuku wa kisasa Milioni 36.9.
“Pamoja na idadi kubwa ya mifugo inaonekana Tanzania ulaji wa nyama upo chini kulingana na viwango vya FAO ambavyo vinamtaka mtu ale kilo 50 kwa mwaka, huku Tanzania ikiwa mtu anakula Kilo 15, hivyo tunahamaisha watu wale nyama kutokana na umuhimu wake ikiwemo viini lishe,”