Top Stories

Lugha ya Kiswahili kupata nafasi kutumika Twitter

on

Watumiaji wa Twitter duniani wataanza kutumia lugha ya kiswahili katika ku-tweet ujumbe katika mtandao huo hii ni kutokana na lugha ya kiswahili kuzungumzwa na kutumika sana Afrika Mashariki na baadhi ya sehemu za Afrika ya kati.

 Hapo awali tweets zilizokuwa zikiandikwa kwa lugha ya Kiswahili zilitambulika kuwa ni lugha inayotumika kutokea Indonesia na kutafsiriwa kama lugha isiyoeleweka kitendo hicho kilisukuma kampeni za mitandaoni zilizoongozwa na Wakenya kwa kutumia hashtags #SwahiliIsNotIndonesian na #TwitterRecognizeSwahili

Hivyo lugha ya Kiswahili inapewa kipaumbele kuwa lugha ya kwanza Afrika kutambulika Twitter ikiwa mtandao huo unatumia lugha 34 na kati ya hizo lugha 34 hakukuwa na lugha yoyote kutokea Afrika.

MWIJAKU “Mc Pilipili ameshindwa kumhudumia mtoto, kimaisha hawezi kunipata”

 

Soma na hizi

Tupia Comments