Tunayo story kutokea kwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk.Hamisi Kigwangalla ambapo amehoji kwanini Tanzania haipati wageni wengi wa Kitalii licha ya vivutio vingi vilivyopo ikiwemo fuvu la Binadamu wa Kwanza (ZINJANTHROPUS).
Akitolea mfano Dk.Kigwangalla amesema kama Misri wana Pyramid na wanapata Watalii kwanini Tanzania ambayo ina fuvu maarufu la Binadamu wa Kwanza ZINJANTHROPUS bado haipati wageni wa kutosha.
“Kwa sisi tuliosoma zamani hakuna asiyejua ZINJANTHROPUS, Dk.Leakey na mke wake Merry ambapo hakuna asitejua duniani lakini licha ya hilo bado hatupati wageni zaidi ya kupata wageni wa Maliasili,”amesema.