Habari za Mastaa

Nuh Mziwanda-“Nawal alinifanya niyumbe kimuziki, nilikosa nguvu”

on

Kwenye kipindi cha Leo Tena cha Clouds FM mwimbaji Nuh Mziwanda amefunguka kuhusu kilichoimbwa ndani ya ngoma yake mpya ‘Natapatapa’ ikiwemo kumzungumzia aliyekuwa mke wake Nawal jinsi alivyobadilika kwenye ndoa ambayo ilidumu kwa miezi mitatu.

‘’Mke wangu Mama Anya alinifanya niyumbe kimuziki, alinichanganya sana, ndoa yangu ilidumu kwa miezi mitatu tu, sikumwelewa nini alichokuwa anakitaka, alikuwa anapenda sana kukesha kwenye vigodoro, nilikuwa nahangaika kumtafuta hadi nikawa sielewi nini kimenipata’’

“Mapenzi ndiyo sababu kubwa ambayo iliniua kimuziki maana wakati nipo kwenye ndoa kuna mambo mengi yalitokea mpaka kufikia hatua ya kuachana na ile mivutano ya hapa na pale baina yangu na aliyekuwa mke wangu ambayo yalinipa stress sana na kukuta napoteza nguvu za kufanya muziki kama zamani na hiyo ndiyo sababu hata iliyopelekea mimi kuandika wimbo wa Natapatapa kwani nimeongelea maisha ambayo nimeyapitia kwenye mahusiano yangu”

“Nilichora tattoo kwa mapenzi na siwezi kufuta na hata watu waliofuta tattoo za wapenzi wao baada ya kuachana nadhani hawakuwa na mapenzi ya dhati na kuna kitu walikuwa wanahitaji na baada ya kupata ndiyo wakafuta, bora nikose mwanamke kuliko kupata mwanamke na kunishawishi kufuta tattoo hizi”

ULIPITWA NA LIVE?:Nikki wa Pili mbele ya RC Makonda ‘Serikali ni mchezaji anayepaisha Penati’

Soma na hizi

Tupia Comments