Habari za Mastaa

The Game amzawadia Mtoto wake wa miaka 16 gari aina ya BMW (+video)

on

Stori kubwa ambayo imeviteka vyombo vya habari nchini Marekani ni kuhusiana na rapper The Game kumzawadia mtoto wake wa kiume Harlem gari aina ya BMW katika sherehe yake ya kuzaliwa ambayo ilifanyika siku ya Jumapili June 30,2019.

Inaelezwa kuwa sherehe hiyo ilihudhuriwa na ndugu,jamaa na marafiki wa karibu wa rapper huyo ambapo wasanii tofauti walipata nafasi ya kutumbuiza kwenye sherehe hiyo. Gumzo limeendelea kutoka kwa mashabiki baada ya umri wa mtoto huyo kuwa ni miaka 16 na wengi kudai kuwa bado ni mdogo kuingia barabarani na kuendesha gari ni bora pesa zilizotumika kununulia gari hilo lingefanyiwa vitu vingine.

Rapper The Game na watoto wake

Rapper The Game ambaye jina lake halisi ni Jayceon Terrell Taylor ana jumla ya watoto watatu, ambapo Harlem ambaye  ndio mtoto wake wa kwanza na aliwahi pia kuonekana kwenye kazi nyingi za baba yake hapo nyuma ikiwemo ngoma ya ‘Celebration’ iliyoachiwa rasmi mwaka 2012 na thamani ya gari aina ya BMW zinatajwa kufikia thamani ya shilingi Milioni 78 za Kitanzania

VIDEO: JAMAA ANAYEFANANA NA JUX ARUSHA “NIKIENDA SEHEMU NAKAA VIP”

Soma na hizi

Tupia Comments