Naibu Waziri wa Mambo Ndani na Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama, Hamad Masauni leo September 26, 2016 ametoa takwimu za ajali za barabarani wakati wa maadhimisho ya kuanza kwa wiki ya Nenda kwa Usalama Mkoani Geita.
Masauni amesema kuwa Taifa linasikitishwa na matukio ya ajali za zinazotokea kila mara huku akieleza kuwa ajali nyingi kati ya zinazotokea husababishwa na uzembe wa madereva na kuzitaka mamlaka za sheria na jeshi la polisi kuwachukulia hatua kali na madhubuti ili kudhibiti hali hiyo.
Akitoa takwimu za ajali zilizotolewa na jeshi la polisi kikosi cha usalama barabarani, Naibu Waziri Masauni amesema kuwa kwa takribani miaka mitatu iliyopita kuanzia mwaka 2013 mpaka kufikia December 2015 kundi lililoongoza kwa kuathirika na matukio ya ajali ni abiria ambao idadi inaonesha kuwa watu 3444 walipoteza maisha, wakiwemo majeruhi 20,181. Kundi la watembea kwa miguu linafatia kwa kusababishiwa vifo vya watu 3328, majeruhi 8256 kutokana na ajali za barabarani.
>>>Wapanda pikipiki ni kundi la tatu likiwa na vifo vya watu 2493, na majeruhi 10,702. Kwa upande wa Baiskeli vifo vilivyotokea ni 1,071 wakati majeruhi wakiwa 2060 na madereva waliofariki kwa ujumla ni 813, majeruhi ni 3,157. Wasukuma mikokoteni 81 walifariki, waliojeruhiwa ni 246. Takwimu hizi zinajumuisha idadi ya ajali 46,536 zilizoripotiwa kwenye vyombo vya sheria ikiwemo jeshi la polisi.
ULIOPITWA NA TAARIFA YA KUUNGUA KWA SHULE YA SEKONDARI MKOLANGA? MKUU WA SHULE AMEZUNGUMZA HAPA