Millard AyoMillard Ayo
  • Top Stories
  • Entertainment
  • Sports
  • Magazeti
  • Contact
Search
  • Contact
  • Blog
  • Complaint
  • Advertise
© 2022 MILLARD AYO. Designed by F&A. All Rights Reserved.
Reading: Rufaa ya Mbowe na Matiko: Mahakama yatoa majibu baada ya Profesa Safari kuhoji (+video)
Share
Notification Show More
Latest News
Breaking: William Ruto atangazwa kuwa Rais Kenya, Shangwe na furaha zaibuka mitaani Nairobi
August 15, 2022
Matokeo ya Urais Kenya kutangazwa leo, Mgombea Ruto awasili Ukumbini Boma ‘Kusubiria matokeo hayo’
August 15, 2022
Live: Matokeo ya Urais nchini Kenya yanatangazwa muda huu
August 15, 2022
Manara na Wana-Yanga wakomaa kuwa kejeli Simba ‘Mlete Mzunguu’
August 15, 2022
Club ya Wolves ya England kuleta makocha wawili Tanzania
August 15, 2022
Aa
Millard AyoMillard Ayo
Aa
  • Top Stories
  • Entertainment
  • Sports
  • Magazeti
Search
  • Top Stories
  • Entertainment
  • Sports
  • Magazeti
Follow US
  • Contact
  • Blog
  • Complaint
  • Advertise
© 2022 MILLARD AYO. Designed by F&A. All Rights Reserved.
Millard Ayo > Blog > AyoTV > Rufaa ya Mbowe na Matiko: Mahakama yatoa majibu baada ya Profesa Safari kuhoji (+video)
AyoTVMixStori KubwaTop Stories

Rufaa ya Mbowe na Matiko: Mahakama yatoa majibu baada ya Profesa Safari kuhoji (+video)

January 3, 2019
Share
2 Min Read
SHARE

Wakati Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko wakiendelea kusota mahabusu, Wakili anyewatetea Profesa Abdallah Safari amehoji katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuhusu rufaa iliyokatwa na upande wa mashtaka katika Mahakama ya Rufani.

Mbowe na Matiko wanasota mahabusu baada ya Mahakama ya Kisutu kuwafutia dhamana yao November 26,2018 kwa kukiuka masharti ya dhamana, ambapo waliamua kukata rufaa Mahakama Kuu lakini iliwekewa pingamizi baada ya upande wa mashtaka kukata rufaa Mahakama ya Rufani.

Profesa Safari alihoji swali moja kuhusu rufaa hiyo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri baada ya Wakili wa Serikali Mkuu, Paul Kadushi kueleza kuwa shauri hilo limeitishwa kwa ajili ya kutajwa.

Baada ya kueleza hayo, Profesa Safari alimuuliza Wakili Kadushi kama rufaa waliyoikata Mahakama ya Rufani ilikuwa chini ya hati ya dharura ama lah na kama haikuwa chini ya hati ya dharura ni kwa nini…?

Katika majibu yake Wakili Kadushi ameeleza kuwa hakuna uhalali wa kisheria kuhusu swali hilo mahakamani hapo, labda lingeulizwa wakiwa Mahakama Kuu ama ya Rufaa.

Kutokana na hatua hiyo, Hakimu Mashauri ameahirisha kesi hiyo hadi January 17,2019 huku akisema swali hilo la rufaa likahojiwe Mahakama Kuu.

Washitakiwa wengine katika kesi hiyo ni Mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msigwa, Mbunge wa Kibamba, John Mnyika, Katibu wa Chadema, Dk. Vincent Mashinji, Mbunge wa Bunda, Ester Bulaya na Katibu wa Chadema Zanzibar, Salum Mwalimu

Wote kwa pamoja wanakabiliwa na mashitaka 13, ikiwemo kula njama, kufanya mkusanyiko wenye ghasia, kuhamasisha hisia za chuki, kushawishi hali ya kutoridhika, uchochezi na kushawishi utendaji wa kosa la jinai kati ya February Mosi na 16, mwaka huu maeneo ya Dar es Salaam.

FULL VIDEO: MBOWE NA MATIKO WALIVYORUDISHWA MAHAKAMANI BAADA YA MWAKA MPYA

You Might Also Like

Breaking: William Ruto atangazwa kuwa Rais Kenya, Shangwe na furaha zaibuka mitaani Nairobi

Matokeo ya Urais Kenya kutangazwa leo, Mgombea Ruto awasili Ukumbini Boma ‘Kusubiria matokeo hayo’

Live: Matokeo ya Urais nchini Kenya yanatangazwa muda huu

Azikwa akiwa hai huko Madaba, DC afika eneo la tukio, ‘Jambo hili ni la kinyama’

Rais Samia atoa Bilioni 15 jimboni kwa Shigongo

TAGGED: Ayo TV, Mix, Stori kubwa, top stories
Mika Ndaba TZA January 3, 2019
Share this Article
Facebook TwitterEmail Print
Share
Previous Article LIVE: Zitto Kabwe anaongea na Waandishi wa Habari
Next Article RC Mwanri aanzisha vita na Walevi “Pombe ina darubini, ulevi ulipojenga nchi!” (+video)
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

You must be logged in to post a comment.

- Advertisement -

Latest News

Breaking: William Ruto atangazwa kuwa Rais Kenya, Shangwe na furaha zaibuka mitaani Nairobi
Top Stories August 15, 2022
Matokeo ya Urais Kenya kutangazwa leo, Mgombea Ruto awasili Ukumbini Boma ‘Kusubiria matokeo hayo’
Top Stories August 15, 2022
Live: Matokeo ya Urais nchini Kenya yanatangazwa muda huu
Top Stories August 15, 2022
Manara na Wana-Yanga wakomaa kuwa kejeli Simba ‘Mlete Mzunguu’
Sports August 15, 2022

You Might also Like

Sports

Club ya Wolves ya England kuleta makocha wawili Tanzania

August 15, 2022
Sports

Inter Milan wawapa Yanga cha kusema, Shaffi Dauda atia neno, Manara apigilia msumari

August 15, 2022
Sports

Barbara awatuliza mashabiki wa Simba, wataka Mzungu aachwe wana mashabiki na mbinu za Kocha

August 15, 2022
Sports

Aziz Ki Mfalme mpya town, mchezo dhidi ya Simba SC ya dhihirissha ubora wake, ‘Jemedari amwagia sifa’

August 14, 2022
Show More
//

To be recognized as Africa’s leading and most trusted online media network providing quality content across all our media platforms by 2025

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

Millard AyoMillard Ayo
Follow US

© 2022 MILLARD AYO. Designed by F&A. All Rights Reserved.

Removed from reading list

Undo

Lost your password?