AyoTV

VIDEO: Mbunge Lwakatare baada ya maamuzi ya Mahakama ya Rufaa

on

Leo August 11, 2017 Mahakama ya Rufaa Tanzania imeyafuta maombi ya kibali cha Mkurugenzi wa Mashtaka (DDP) kutaka kupinga uamuzi wa Mahakama Kuu kufuta shtaka la ugaidi lililokuwa linamkabili Mbunge wa Bukoba Mjini, Wilfred Lwakatare.

Baada ya uamuzi huo wa Mahakama ya Rufaa, Lwakatare alisema anamshukuru Mwenyezi Mungu kwa hatua hiyo kwa kuwa hakulitenda kosa hilo akidai kwamba lilitengenezwa.

>>>”Kama ilivyozungumzwa ndani ya Mahakama ya Rufaa mbele ya Jaji Kipenka kwa upande wa Serikali ndio ilikuwa imekata  rufaa dhidi ya maamuzi ya Jaji Kaduli ya kuniachia huru kwenye kosa la kufanya njama za Ugaidi.

“Kimsingi namshukuru Mwenyezi Mungu kwa sababu kama ilivyokuwa tangia awali na jinsi Mahakama Kuu ilivyokuwa imeona hakukuwepo na njama zozote. Ilikuwa ni mipango tu iliyokuwa imepengwa hata sielewi kwa sababu zipi.” – Wilfred Lwakatare.

Kwenye hii video hapa chini kuna kila kitu…tazama kwa kubonyeza PLAY!!!

Manji amkataa Wakili Kibatala kusimamia kesi yake…tazama hapa!! 

Soma na hizi

Tupia Comments