Premier Bet SwahiliFlix Ad Tigo Ad

Habari za Mastaa

Amber Rutty arudishwa Mahakamani Kisutu akosa tena dhamana

on

Msanii Rutyfiya Abubakary maarufu kama ‘Amber Rutty’ na mpenzi wake Said Bakary wamekosa tena kudhamaniwa katika kesi inayowakabili ya kufanya mapenzi kinyume na maumbile katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa sababu wadhamini wao hawajafika.

Mbali na Amber Ruth na Said Bakary, mshtakiwa mwingine ni James Charles maarufu kama ‘James Delicious’ ambaye yeye yupo nje kwa dhamana.

Wakili wa serikali Mwanaamina Kombakono amemueleza Hakimu Mkazi Mkuu, Augustine, Rwezire kuwa kesi hiyo imeitishwa kwa ajili ya kutajwa na upelelezi, haujakamilika.Baada ya kueleza hayo, Amber Rutty aliieleza mahakama kuwa wadhamini wake wapo hivyo anaomba adhaminiwe.

Hata hivyo, Hakimu alipouliza wadhamini wa Amber Rutty wapo wapi hakuna aliyejitokeza ambapo amemwambia endapo wakifika watafata taratibu ili wamdhaminiwe.Kesi imeahirishwa hadi November 26,2018.

Washtakiwa hao wanakabiliwa na makosa manne ikiwemo kufanya mapenzi kinyume na maumbile ambalo linamkabili Amber Ruth, ambapo anadaiwa amelitenda kati ama baada ya October 25, 2018 ambapo alimruhusu Said Bakary kumuingilia kinyume na maumbile, kosa ambalo amelikana.

Kosa la tatu la kuchapisha video ama picha za ngono, ambapo linamkabili James Charles ama James Delicious akidaiwa kati ya October 25,2018 alisambaza video za ngono kupitia magroup ya Whatsapp.

Ili Amber Rutty na mpenzi wakewadhaminiwe wanatakiwa kutimiza masharti yavkuwa na wadhamini 2 ambapo kila mtu atasaini bondi ya Shilingi Milioni 15, pia wadhamini wawe na vitambulisho vya taifa.

BREAKING NEWS: MBOWE ALIVYOWASILI MAHAKAMANI KISUTU

Soma na hizi

Tupia Comments