AyoTV

Watanzania Milioni 30 wanavyokosa Maji Vijijini, Serikali yatoa kauli (+video)

on

Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Makame Mbarawa amesema serikali imepewa jukumu la kuhakikisha miji ya mikoa upatikanaji wa maji unafikia asilimia 95, huku miji ya wilaya inafikia asilimia 90 na vijijini ifikie asilimia 85.

Akizungumza na waandishi wa habari Profesa Mbarawa amesema kutokana na hatua hiyo serikali imeanza kutekeleza miradi mbalimbali ya maji kuanzia mwaka 2006 ambapo hadi sasa miradi 1801 imeshatekelezwa, huku inayotekelezwa sasa ni 500.

Amesema baada ya utekelezwaji huo katika miji ya mikoa upatikanaji umefikia asilimia 75, huku vijiji wakiwa asilimia 59.08 ambapo kuna miradi mingine ilikamilika takribani vituo Laki Moja na kama ingefanya kazi Watanzania Milioni 30 wangepata maji safi na salama.

“Vituo vinavyotoa maji ni Elfu themanini na tano ambapo sababu kuu ni kwamba ubadilikaji wa hali ya hewa kwani baadhi ya maeno maji yanakauka kutokana na kutotunzwa kwa vyanzo vya maji,”amesema.

ANAYEDAIWA KUMHONGA WAZIRI LUKUVI MILIONI 90 ALIVYOACHIWA HURU

Soma na hizi

Tupia Comments