Stori Kubwa

“Madereva wa serikali nawapiga Pingu, mahakamani, tunawaondolea sifa”-Kamanda Muslim

on

Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Fortunatus Muslim amesema akikamata madereva wa serikali wanaovunja sheria atawapiga Pingu kisha kuwafikisha mahakamani na wakitoka huko atawaondolea sifa.

Kamanda Muslim ameyasema hayo wakati akiwa kwenye Oparesheni ya kuhakikisha barabara zinakuwa salama na kuepusha ajali ambazo sio za lazima, hasa zinazosababishwa na magari ya serikali ambapo madereva wengi wa serikali wanaonekana wapo juu ya sheria.

“Madereva wengi hamtaki kufata sheria wala alama za barabarani mnaendesha mwendokasi hata mkisimamishwa nyie mnawasha taa, muda mwingine viongozi wanakuwa ndani ya hayo hayo magari na wanalipia faini,”amesema.

Kutokana na hatua hiyo, amesema wanajaribu kuyafatilia kwa karibu magari ya serikali kwani hawataki kupoteza wataalamu ambao serikali imekuwa ikiwaandaa kwa muda mrefu.

“Sasa hivi tukiwakamata tunawapiga pingu, tunawaweka ndani kisha mahakamani na ukitoka mahakamani naondoa sifa ya kuendesha magari ya serikali uende kuendesha magari mengine,”amesema.

BAJAJI ILIYOBUNIWA TANZANIA BADO HAIJAREKEBISHWA ‘NIMEKATISHWA TAMAA’

Soma na hizi

Tupia Comments